Movie ya La La Land kwa mara nyingine tena imefanikiwa kuandika historia baada ya kutajwa kuwania tuzo kwenye vipengele 14 vya tuzo za Oscars.

Mastaa wa movie hiyo, Ryan Gosling na Emma Stone wamechaguliwa kuwania tuzo za ‘best actor na best actress’.

Kuchaguliwa kwa La La Land kwenye vipengele 14 kumeifanya filamu hiyo kufikia rekodi za filamu za All About Eve na Titanic ambazo zote zilichaguliwa kwenye vipengele 14 mwaka 1951 na 1998.

Pamoja na historia hiyo, pia La La Land imeweka historia ya kuwa filamu ya muziki iliyotajwa kwenye vipengele vingi zaidi ikizipita Mary Poppins na Chicago zilizowahi kutajwa kwenye vipengele 13.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *