Beki wa Tottenham, Kyle Walker amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo ambao utamuweka hapo mpaka msimu wa mwaka 2021.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26 alijiunga na Tottenham msimu wa mwaka 2009 na mpaka sasa ameichezea mechi 150 klabu hiyo.

Baada ya kusaini mkataba huyo Walker amewashukuru wapenzi na mashabiki wa klabu kutokana na sapoti wanayoipa timu yao pamoja na kuhaidi kuitumikia Tottenham kwa moyo wake wote.

Walker anaungana na wachezaji wenzake Danny Rose, Christian Eriksen, Eric Dier, Dele Alli, Harry Winks na Tom Carroll ambao tayari wameshasaini mikataba mipya ndani ya klabu hiyo.

Tottenham inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi nchini Uingereza baada ya kucheza mechi tano na kushinda tatu na kutoka sare mechi mbili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *