Chama cha soka cha Ghana kimemteua tena Kwesi Appiah kuwa kocha mkuuwa wa timu ya taifa ya Ghana (Black stars).

Appiah amepewa mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu ya taifa na ataanza kazi yake rasmi mei mosi mwaka huu.

Kocha huyu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Avram Grant amabe alijiuzulu baada ya kumalizika kwa fainali za michuano ya kombe la mataifa ya afrika ya mwaka 2017.

Hi ni mara ya pili kwa kocha huyu kuinoa timu hiyo taifa mara ya kwanza aliiongoza timu hiyo kuanzia mwaka 2012 mpaka 2014.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *