Mshambuliaji wa Gabon na mwanasoka bora wa zamani wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang anaamini kuwa kutolewa kwenye hatua ya makundi kwa wenyeji hao wa AFCON kumetokana na kukosa maandalizi ya kutosha ya pamoja ya kikosi hicho.

 Gabon walitakiwa kuwafunga Cameroon kwenye mechi ya mwisho ili kuweza kufuzu lakini waliishia kupata suluhu ya 0-0.

Aubameyang alikariirwa akisema: ‘Inakera sana kwasababu tulipata nafasi. Inasikitisha kwasababu zipo siku ambazo mtu unakosa bahati, ni kama nilivyoshindwa kufunga nikiwa umbali wa mita mbili’.

‘Tumefadhaishwa sana. Hatukuwa na muda wa kutosha wa kuwa pamoja kwaajili ya mashindano’.

‘Tulikuwa na kikosi imara zaidi kwenye kundi ingawa kubadilisha kocha dakika za mwisho na kuchelewa kuanza maandalizi kwa siku kadhaa kulituathiri. Hata hivyo ninajivunia kwa kikosi chetu na kwakuwa nafahamu kila mmoja alitoa kila alichoweza kwaajili ya taifa’.

Gabon walikuwa kundi A pamoja na Cameroon, Burkina Faso na Guinea na timu zilizofuzu kwa mzunguko wa pili ni Cameroon na Burkina Faso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *