Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz anaonekana kuchukua kasi kubwa ya kuwachukua wasanii wachanga na wakongwe ambao wamekosa menejimenti za uhakika za kuwasaidia kufika mbali zaidi.

Hivi karibuni lebo ya Diamond Platnumz, WCB ilimsainisha kwa miaka 10 staa Rich Mavoko huku mitazamo ya wadau wa muziki ikiendelea kutofautiana juu ya uamuzi huo.

Lakini, je? Diamond Platnumz amejifunza wapi biashara ya kusimamia wasanii wa muziki? Je, ni yeye anayewasimamia au kuna watu wanaofanya shughuli hiyo kupitia Diamond (kutokana na jina lake)

Lakini je, Diamond Platnumz anafahamu kuwa biashara hiyo ni pasua kichwa?

Mkongwe wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya a.k.a AY aliwahi kuifanya biashara hiyo miaka ya nyuma na moja ya wasanii aliowahi kuwasimamia ni Ommy Dimpoz pamoja na Feza Kessy lakini kwa sasa ameachana kabisa na biashara hiyo, kwanini?

AY anadai kuwa iwapo msanii aliyechini ya lebo fulani akawa hana upeo mkubwa wa ufahamu wa masuala ya biashara basi kazi hiyo huwa ngumu sana kwa menejimenti yake kwakuwa moja kati ya hatari zinazojitokeza ni msanii wa aina hiyo anapolaghaiwa na watu wengine (baada ya menejimenti yake kufanya juhudi kubwa ya kumtengeneza na kumtengenezea jina) na kuamua kuondoka kinyemela.

Diamond na WCB mmejipanga kwa hilo?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *