Staa wa lebo ya RockaStar4000, Barakah The Prince amefunguka ukweli wa mambo kuwa hakutarajia ngoma yake ya NISAMEHE kufanya vizuri sokoni kama ilivyotokea.

Barakah ameweka wazi kuwa kwa namna ‘team’ zilivyotawala soko la nyumbani ilikuwa ni risk kubwa kufanya kazi na Ali kiba kwasababu alitarajia baadhi ya mashabiki ambao wanaendekeza u-team wasingeiunga mkono ngoma hiyo licha ya ubora wake.

Japokuwa ni dhahiri kuwa Ali Kiba ni staa anayefanya kazi nzuri na anakubalika kimataifa lakini kwa soko la nyumbani hali imekuwa tofauti kwasababu ya kundekeza upinzani usio na manufaa kwenye muziki.

‘Nashukuru sana kwakuwa ngoma imefanya vizuri lakini ninakiri kuwa ilikuwa ni risk ambayo ilikuwa ni lazima kuichukua’.

Je, wasanii wengine waanze kujiuliza mara mbili kila wanapotaka kufanya kazi na mastaa hawa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *