Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kusah amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuachia wimbo baada ya kusema kuwa anashauku ya kurudi kazini.

Kusah amesema kuwa yupo tayari kuwafurahisha mashabiki zake kwa kurudi kazini na wimbo mpya,japo hajaweka wazi ni lini na anarudi na wimbo gani atakaouachia ila ni ishara nzuri kuwa wimbo upo tayari pamoja na video yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kusah amepost kipande cha video na kuandika “Nina shauku na Furaha ya kuwaambia kwamba “NARUDI KAZINI.

Mwanamuziki huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia kazi mpya hivyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa kupokea preject yake mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *