Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kusah amefunguka na kusema kuwa ameamua kuja tofauti kwenye uimbaji kutokana na wasanii kuigana kuimba.

Kusah mesema kuwa ameamua kubadilika katika wimbo wake mpya uitwao Wasawasi kwa kuwa Wasanii wanafanana sana kwenye muziki na alikuwa akijitahidi kuimba kama kawaida alikuwa akiona vinafanana na wengine hivyo akaona aje na Style mpya.

Mbali na hivyo amesema kuwa wimbo huo una uhalisia kwa sababu kwenye Mapenzi lazima kuwe na Wasiwasi kati ya wapendanao hivyo wimbo huo una ujumbe tosha.

Kusah amaechia Ngoma mpya Wasiwasi ambapo umo ndani ameimba tofauti na wengi walivyomzoea, Amefunguka sababu za kubadilika katika Ngoma hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *