Mpenzi wa muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel, Kusah ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, amekanusha taarifa kuwa amepigana kugombea mwanamke mkoani Singida.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja kufuatia taarifa kusambaa mtandaoni kuwa aligombana kisa mwanamke jambo ambalo amelipinga vikali.

Kusah amesema ameiona hiyo story na hakuna ukweli wowote bali wanawake hao walikuwa wanarekodi naye video kupitia mtandao wa Snapchat.

‘Hata mimi nashangaa kusikia habari hizo napenda kuwahakikishia mashabiki wangu kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote katika maisha yangu’ Alisema Kusah

Kusah kwasasa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Aunty Ezekiel baada ya kuachana na Ruby ambaye amezaa nae mtoto mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *