Kundi la The Heroes ambalo lilishiriki Dance100% mwaka huu na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na hatimaye kushindwa kufuzu fainali limesema litaimarisha kundi lao ili kuendelea kushiriki kazi nyingine.

Akizungumza kwa niaba ya mwenzake Emmanuel Dickson amesema wameshiriki mara ya tatu hivyo wameweza kujenga umoja hadi sasa na ndiyo maana mwaka huu wakaweza kushiriki bila tatizo.

Dickson amesma kuwa wameshiriki mara ya tatu na hata baada ya kushindwa bado shughuli za kucheza wanafanyia Gongo la Mboto na wataendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali na ikitokea tukio bado watafanya na wanajipanga vya kutosha Dance100% ijayo.

Shindano la Dance100% limefikia hatua ya fainali mbapo makundi kwa sasa yanaendelea na maandalizi ambapo yatachuana makundi matano yaliyoshinda hatua ya nusu fainali ili kundi moja liweze kuibuka na ushindi.

Kundi litakaloibuka na ushindi mwaka huu kuibuka na kitita cha milioni 7 kwenye shindano hilo linaloendelea jijini Dar es Salaam.

Makundi yaliyoingia fainali ni

  1. BBK Boys
  2. Team Makorokocho
  3. Wazawa Crew
  4. Clever Boys
  5. D.D.I Crew

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *