Kundi la Tatanisha Crew  limesema linaridhishwa na majaji wa shindano la Dance100% kwani wanatoa alama vizuri bila kuwa na upendeleo wowote kulingana na uwezo wa kundi.

Mwenyekiti wa kundi hilo Thomas Paul amesema kitendo cha majaji kuwa na maamuzi sahihi na kueleza kila kundi wapi limefanya vizuri na vibaya kumewafanya kuwa na imani kubwa na majaji hao.

Pia mwenyekiti huyo amesema wao wanafanya mazoezi kwa hali ya juu kujiandaa na hatua ya nusu fainali kwa kuwa wana imani kubwa na majaji kwamba wanatenda haki kulingana na kundi linavyoonesha uwezo.

Jaji Nyamwela: Akiwa na amajaji wenzake kwenye shindano la Dance 100#
Jaji Nyamwela: Akiwa na amajaji wenzake kwenye shindano la Dance 100.

Kwa upande mwingine Jaji Super Nyamwela amesema katika shindano la Dance100% hakuna upendeleo wowote na makundi yote yapo sawa na yameshaelezwa vigezo ambavyo vinatakiwa.

Nyamwela amesema kwamba hakuna kundi ambalo linaweza kusema kuna upendeleo kwa kuwa mambo yote wameshawaeleza na kuwafundisha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *