Kundi la D.D.I Crew limesema kuwa limejiandaa vya kutosha kwa ajili ya fainali ya mashindano ya Dance100% zitakazofanyika Septemba 24 mwaka huu.

2016 ambazo zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam limesema kuwa kundi hilo ni dogo kiumri ila ni wakubwa kiakili.

Mwenyekiti wa kundi hilo Samson Shobigo amesema kuwa kundi hilo limejipanga vizuri katika kunyakua kitita cha milioni 7 na tayari wana mikakati ya kutumia fedha hizo katika miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti huyo amesema “Sisi tumejipanga vyema katika kushiriki fainali Jumamosi na sisi ni wazoefu katika mashindano ya kucheza, tumeshakwenda hadi nje ya nchi kwa ajili ya shughuli ya dansi, hivyo watu wakae mkao wa kushuhudia mambo mazuri sana kutoka kwetu.

Kwa upande wake binti pekee anayeshiriki Shindano la Dance100% maarufu kwa jina la Kibibi amewataka kinadada kutoogopa kutumia fursa zinapojitokeza kwani kupitia Dance100% inamfanya atambulike kwa kipaji alichonacho ndani ya jamii.

Fainali za mashindano ya Dnce 100% zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba 24 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *