Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ruby amesema kwamba hakwenda mkaoani Mwanza kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta licha ya kusajiliwa na Clouds Media kwasababu waandaji hulipa fedha ndogo.

Ruby amedai kuwa kutolewa kimuziki na Clouds Media hakumaanishi kuwa ataendelea kuwatumikia kama wanavyotaka kwakuwa naye ana maisha yake kwa sasa nje ya kampuni hiyo.

Staa hyuo amesema show ya Fiesta ni kubwa kuliko maslahi wanayolipa na kwamba yangemwacha katika wakati mgumu kuandaa show yake mwenyewe.

ruby (1)

Ruby alipatikana kupitia shindano la Supa Diva mwaka 2014 liliondaliwa na Clouds kupitia tamasha la Fiesta na kusainishwa chini ya kampuni ya THT inayomilikiwa na mkurugeniz wa vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *