Shirikisho la Soka nchini (TFF), limeshusha bei ya kiingilio katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Taifa Stars na Botswana utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo imesema punguzo hilo litakuwa ni kwa watu watakaokaa mzunguko kutoka Sh 5,000 hadi Sh. 3,000.

Pamoja na punguzo hilo kwa mashabiki wa mpira wa miguu watakaoketi Majukwaa Maalumu – VIP “A” watalipia Sh 15,000 na wale watakaoketi VIP “B” na “C” watalipia Sh 10,000.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga kwa upande wake aliwathibitishia Waandishi wa Habari kwamba kikosi chake kiko imara kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa 10.00 jioni.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Botswana amesema kwamba anatarajiwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa sababu amegundua kuwa kikosi cha Taifa Stars kina vijana wengi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *