Polisi nchini Malaysia wamemkamata mwanamke mmoja kuhusiana na mauaji ya ndugu wa wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Polisi wanasema mwanamke huyo amekamatwa katika uwanja wa ndege uliopo katika mji mkuu Kuala Lumpur ambapo Kim Jong-nam alishambuliwa.

Mwanamke huyo alikamatwa muda wa saa mbili na nusu asubuhi leo kwa saa za Malaysia baada ya kutokea tukio hilo la mauaji.

Mshukiwa huyo alitambuliwa kwa kutumia video za kamera za siri, CCTV, katika uwanja wa ndege na alikuwa peke yake wakati wa kukamatwa kwake.

Ametambuliwa kama Doan Thi Huong, aliyezaliwa 31 Mei 1988, kwa mujibu wa pasipoti aliyokuwa nayo.

Picha za CCTV ambazo zinasambazwa kwenye vyombo vya habari zinawaangazia wanawake wawili ambao walikuwa wameambatana na Bw Kim, na ambao muda mfupi baadaye walionekana wakiondoka eneo hilo kwa kutumia teksi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *