Australia imesema kuwa imepokea barua kutoka Korea Kaskazini ikiitaka serikali hiyo kutojihusisha na utawala wa Rais Trump ambayo imekuwa katika mvutano kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Waziri mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia imetumwa katika mataifa mbalimbali kwaajili ya shinikizo la kutoiunga mkono Marekani ambayo imekuwa ikishawishi kuwekewa vikwazo Korea Kaskazini.

Aidha, amesema inaonyesha kuwa shinikizo la kidiplomasia lililotolewa na Marekani dhidi ya Korea Kaskzini limeanza kufanya kazi,ingawa barua hiyo kwa sehemu kubwa imejaa malalamiko kuhusu Australia kushirikiana na serikali ya Trump.

Turnbull amesema kuwa “Wametutumia barua hii kwaajili ya kututaka tusishilikiane na utawala wa Trump, lakini tumegundua kuwa barua hizi zimetumwa katika mataifa mengine mengi, nadhani lile agizo la kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini sasa limeanza kufanya kazi,”.

Hata hivyo, Korea Kaskazini imekiuka makubaliano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni baada ya kuanza kufanya majaribio ya makombora mbali mbali ya masafa marefu ambayo baadhi yake yalipita katika anga la Japan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *