Nchi ya Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora.

Kombora hilo limeonekana likianguka katika bahari ya Japan kulingana na chombo cha habari cha kitaifa cha Japan.

Mapema mwezi Julai, Pyongyang ilidai kufanikiwa kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza.

Kombora hilo ni la hivi karibuni katika msururu wa makombora yaliofanyiwa majaribio hatua inayokiuka marufuku ya UN.

Umbali wake umepingwa lakini wataalam wanasema kuwa linaweza kufika Alaska nchini Marekani.

Msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema kuwa kombora hilo lilirushwa na kwamba habari zaidi zinasubiriwa.

Kombora hilo lilirushwa kutoka mkoa wa Jagang kaskazini mwa taifa hilo , kulingana na chombo cha habari cha Korea kusini Yonhap.

Katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan Yoshihide Suga alisema kuwa kombora hilo lilisafiri kwa takriban dakika 45 ikilinganishwa na kombora la masafa marefu lililofanyiwa majaribio mapema mwezi Julai.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameitisha mkutano wa kiusalama katikati ya usiku kulingana na Yonhap

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *