Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora ya masafa marefu mashariki mwa pwani ya nchi na kuzua shtuma za kimataifa.

Korea Kusini imesema kuwa hiyo ilionyesha tamaa ya Korea Kaskazini kushambulia majirani zake huku Japan ikidai kuwa kombora hilo lilianguka katika bahari ya Japan.

kombora

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ametaja kitendo hicho kuwa cha uchokozi na tishio kubwa kwa usalama wa Japan.

Marekani imesema kuwa makombora mawili yalifyatuliwa lakini moja likalipuka muda mfupi baada ya kufyatuliwa huku ikisema kuwa iko tayari kujilinda pamoja na washirika wake.

Jaribio hilo ndilo la hivi punde linalokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *