Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limebadilisha muda wa kufanyika kwa Kombe la mataifa Afrika ambapo sasa litafanyika mwezi Juni na Julai.

Mchuano huo huwa unafanyika mnamo mwezi Januari na Februari na kusababisha migogro na vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.

Kinyang’anyiro hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon kitashirikisha timu 24 badala ya 16.

Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.

Upanuzi wa mechi hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon ambayo itaanda fainali ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya kati akilazimika kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.

Caf ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu mataifa kutoka mabara mengine kushiriki ama hata kuandaa mchuano huo.

Tangazo hilo linajiri kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na rais wa Caf Ahmad kuzungumzia hali ya soka barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *