Mwanamuziki wa Jamhuri wa Kidemokrasi ya Kongo, Koffi Olomide ameomba radhi tena kufuatia tukio la kumpiga teke dansa wake alipokuwa kwenye uwanja wa ndege nchini Kenya.

Koffi Olomide amejitokeza kupitia kipindi cha Churchill Show kinachooneshwa katika kituo cha runinga cha NTV na kuwaomba msamaha Wakenya na mashabiki wake kwa ujumla kwa kitendo hicho.

Nguli huyo wa wa muziki wa Rhumba alikamatwa nchini Kenya mwezi Julai mwaka huu na kurudishwa nchini Congo baada ya kumpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa ajili ya tamasha.

Koffi anadaiwa kufanya tukio hilo baada ya Pamela kukorofishana na mwanamuziki wake aitwaye Cindy Le Couer ambaye ni mpenzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *