Staa wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa nchini humo.

Olomide alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonesha akimpiga teke mchezaji wake wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta baada ya kuwasili kwa ajili ya tamasha nchini humo.

Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hilo likaahirishwa kutokana na tukio hilo.

Waandalizi wa tamasha ambalo Olomide alipangiwa kutumbuiza nchini Zambia pia walitangaza kwamba wamefutilia mbali hafla hiyo kutokana na yaliyotokea Nairobi nchini Kenya.

Mwanamuziki huyo, aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumapili, aliomba radhi mashabiki wake na hasa “wanawake na watoto”.

Olomide pia aliomba msamaha kutoka kwa raia wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao huenda alihisi kwamba tabia yake iliwakosea heshima.

Koffi Olomide: Akikamatwa na polisi nyumbani kwake jijini Kinshasa, Jamhuri ya kidemokrai ya Congo.
Koffi Olomide: Akikamatwa na polisi nyumbani kwake jijini Kinshasa, Jamhuri ya kidemokrai ya Congo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *