Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela kwa kosaa la kumpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela akiwa nchini Kenya.

Koffi Olomide amehukumiwa muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa nchini Congo.

Koffi alikana tuhuma za kumpiga dansa huyo na mwanasheria wake aitwaye George Wajackoyah naye amelaani kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa wakati wa kumkamata.

Nguli huyo wa wa muziki wa Rhumba alikamatwa nchini Kenya Ijumaa iliyopita na kurudishwa nchini Congo baada ya kumpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa ajili ya tamasha.

Koffi anadaiwa kufanya tukio hilo baada ya Pamela kukorofishana na mwanamuziki wake aitwaye Cindy Le Couer ambaye ni mpenzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *