Baada ya mwanamuziki, Koffi Olomide kukamatwa Jumanne nyumbani kwake Kinshasa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya.

Baadaye ikawa imeripotiwa kuwa amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa na faini.

Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali.

Shirika la utangazji la BBC limeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

 Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini  Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo  na kusema  kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *