Aliyekuwa kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm ametangazwa kuwa kocha mkuu wa Singida United iliyopanda daraja msimu huu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa za kujiunga na klabu hiyo kwa kocha huyo zilianza kusambaa jana katika mitandao ya kijamii lakini leo imekuwa kweli.

Kocha huyo aliachishwa kazi katika klabu ya Yanga na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Lwandamina kutoka Zambia.

Baada ya kutolewa nafasi hiyo ya ukocha wa Yanga, Hans Van Pluijm alichaguliwa kuwa mkurugenzi wa Yanga ambapo hakuduma sana na kuondolewa kutoka na ukata wa kifedha katika klabu ya Yanga.

Hans van Pluijm akiwa na Yanga ameshinda mataji ya FA na Ligi Kuu msimu uliyopita sambamba na kuifikisha hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika kabla ya kutolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *