Kocha mkuu wa Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC, Hans van Pluijm ameielezea ratiba mpya ya Ligi Kuu iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini “TFF” na kusema kuwa bado timu yake ina nafasi ya kutetea ubingwa huo.

Ratiba hiyo inaonesha Yanga itaanza kucheza mechi ya kwanza dhidi ya JKT Ruvu kwenye mechi ya ligi kuu itakayofanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 31 mwaka huu.

Pluijm amesema anajua ligi ya msimu ujao itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu nyingi kujipanga kwa kufanya usajili mzuri lakini bado timu yake ina nafasi ya kutetea taji hilo kwa mara ya tatu kutokana na ubora wa wachezaji aliokuwa nao.

Kocha huyo ambaye bado ajasaini mkataba mpya na timu hiyo aliongeza kwa kusema kama kocha angependa kuendelea kuifundisha timu hiyo kutokana na mafanikio makubwa

aliyoyapata katika kipindi cha msimu mmoja na nusu tangu aliporejea kuifundisha kwa mara ya pili kwa hiyo atakutana na Mwenyekiti wa Yanga, yusuf Manji kwa ajiri ya kuzungumza kuhusu kusaini mkataba mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *