Kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Fernando Santos amesaini mkataba mpya wa miaka minne umbapo utamuweka katika timu hiyo mpaka mwaka 2020.

Chama cha soka nchini Ureno “FPF” kimemuongezea mkataba kocha huyo baada ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kutwaa taji la michuano ya Ulaya iliyomalizika nchini Ufaransa mwanzoni mwa mwezi huu.

Kocha huyo pia aliwahi kuzifundisha timu za Benfica, Porto na Sporting Lisborn zote za Ureno pamoja na timu ya taifa ya Ugiriki, alinza kuifundisha timu ya taifa ya Ureno toka mwaka 2014.

Mkataba wake mpya alioongezwa utamfanya kukiongoza kikosi hicho katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi na ile ijayo ya Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *