Kocha mkuu wa Azam FC, Zeben Rodriguez amesema kwamba Ligi Kuu ya msimu huu itakuwa ngumu na anahitaji muda zaidi ili kutengeneza timu ya ushindani kwenye kikosi hiko.

Kocha huyo amesema anahitaji muda zaidi ili kukisuka kikosi chake na kucheza kupitia mifumo wanayoendelea kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es Salaam.

Rodriguez amesema ameshuhudia mechi za kwanza za ligi msimu huu na kudai kuwa haitakuwa ligi rahisi sana na ngumu kwake yeye kutokana na kikosi alichonacho kwasasa.

Zeben pia ametanabaisha kuwa atayafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya African Lyon uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi na kumalizika kwa sare 1-1.

Azam FC inatarajiwa kucheza mechi yake ya pili ya ligi kuu Tanzania dhidi ya Majimaji kutoka Songea.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *