Kocha mkuu wa timu ya Thika United, James Nandwa amesema anaamini usajili wa mshambuliaji raia wa Nigeria Ichi Chibueze utasaidia timu hiyo kwenye janga la kushuka daraja kwenye ligi kuu nchini Kenya.

Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa wachezaji watatu waliosajiliwa na timu hiyo kipindi cha dirisha la usajili ambapo alikuwa anacheza katika timu ya Shabana FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Kenya.

Kocha Nandwa amesema mshambuliaji huyo ameanza mazoezi na anamatumaini atazoeana na wachezaji wenzake katika kikosi hiko ambacho kinaepuka janga la kushuka daraja.

Kocha huyo ameongeza kwa kusema Chibueze ni mshambuliaji mzuri na anaamini ataleta mabadiliko katika timu hiyo.

Thika United inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Kenya inayoshirikisha timu 16 ambapo mbili ushuka daraja, ni tofauti ya alama tatu kati ya Thika United na Nairobi City Stars amabyo inashika nafasi ya 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *