Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa ameumizwa kwa timu yake kukubali kipigo cha kizembe cha mabao 2-0 dhidi ya Leicester City.

Klopp ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa michuano ya Carabao Cup na kukubali kipigo cha mabao hayo 2-0 dhidi ya Leicester katika dimba la King Power hapo jana siku ya Jumanne.

“Nimeumizwa mno kwa namna tulivyofungwa kizembe tumeshindwa kushinda katika michezo mitatu sasa, Liverpool imemiliki mpira katika kipindi chote cha kwanza”, Klopp ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Klopp ameongeza kuwa  “Leicester angalau walidumu katika mchezo kutokana hatukuwa vizuri lakini tulipaswa kuendelea kuwa ndani ya mchezo hadi mwisho na kutoruhusu mabao, wametufunga kirahisi mno”.

“Kuusimulia mchezo huu ni rahisi mno kwakuwa tulikuwa wazuri na kuwazidi katika kipindi cha kwanza licha yakuwa tulishindwa kutumia nafasi vizuri na kupata bao lakini wakati mwingine hii ni sehemu ya mchezo”.

Meneja huyo aliyeleta mabadiliko makubwa tangu  ajiunge na klabu hiyo  ameongeza kuwa “Tumecheza mpira mzuri katika dakika 45 za kipindi cha kwanza na tungeamua matokeo katika kipindi hicho  tumepata nafasi zakutosha  lakini mpira ni dakika 90”.

Waliyoibuka mashujaa kwakuipatia ushindi Mbweha hao wenyeji wa King Power ni wachezaji, Shinji Okazaki na Islam Slimani ambao wameisaidia  klabu ya Leicester  kutinga raundi ya nne ya michuano hiyo ya Carabao Cup

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *