Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza imekamilisha usajili wa beki wa kati, Ragnar Klavan kutoka timu ya Augsburg inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani ‘Bundersliga’.

Klabu hiyo imelipa kiasi cha paundi milioni 4.2 kwa naodha huyo wa Estonia aliyecheza mechi zote mbili kwenye michuano ya Europa ligi dhidi ya Liverpool msimu uliopita.

Kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp amemsajili beki huyo ili kuziba pengo lililopo baada ya kuachwa kwa beki Kolo Toure, kuumia kwa beki wake Mamadou Sakho na kuuzwa kwa beki Martin Skrtel aliyejiunga na Fenerbahce ya nchini Uturuki wiki iliyopita.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *