Klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana imepeata ajali mbaya ya gari wakati ikitoka kwenye mechi katika mji kuu wa Accra.

Timu hiyo ilikuwa inarejea katika mji wake ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo , Kumasi baada ya mchezo wa ligi kuu mjini Accra dhidi ya Inter Allies FC.

Image caption Asante Kotoko ni miongoni mwa klabu zinazotoa upinzani mkubwa Afrika

Ajali hiyo imetokea katika sehemu iitwayo Nkawkaw kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ghana, Accra.

Inasemekana kuwa baadhi ya wachezaji wameumia vibaya akiwemo pia kocha wa timu hiyo na pia kuna kifo cha mtu mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *