Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa wastani wa asilimia 1.4 kutoka asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Februari hadi asilimia 6.4 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya sababu zilizochangia ongezeko hilo ni kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Vyakula vilivyopanda bei ni pamoja na mchele, sukari, unga wa mahindi, mtama, ndizi pamoja na mihogo mibichi.

Kufuatia ongezeko hilo, baadhi ya wakazi Jijini Dar es Salaam wametaja ukosefu wa kipato kuwa unaongeza ugumu wa maisha hasa kwa wafanyabiashara ambao wamelalamikia upungufu wa wateja sambamba na ushauri wa hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.

Ripoti hiyo ya ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) zinazobainisha kuwa kasi ya mfumuko ya bei imekuwa ikiongezeka mwezi hadi mwezi kutoka asilimia 4.8 nNovemba mwaka jana hadi asilimia 6.4 hadi mwezi Machi mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *