Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha kuzalisha Konyagi, Tanzania Distilleries kilichopo Chang’ombe na kukuta bado kinazalisha pombe aina ya viroba.

Makamba aliongozana na timu ya watu kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Jeshi la Polisi na Baraza la Mazingira (NEMC).

Katika ukaguzi huo walikuta shehena yenye katoni zaidi ya 100,000 ya viroba vya konyagi na valuers vilivyoonyesha kuendelea kuzalishwa hadi jana ikiwa ni siku ya mwisho ya tangazo la katazo la kuzalisha pombe hiyo.

Pia wamebaini sehemu ya mitambo zilipokutwa pombe hizo zilionyesha mtambo huo umezimwa ghafla huku pombe ikimwagika sakafuni, hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho walikuwa wanalazimisha kuwasha CCTV ili kuwaonyesha mitambo hiyo ilizimwa lini.

Meneja wa kiwanda hicho Davis Deogratius, amegoma kusaini fomu ya idadi ya mzigo aliokutwa nao hadi alipolazimishwa na hatimaye kukubali ambapo, alilalamikia hatua hiyo huku akieleza hasara watakayoipata kutokana na kutouza mzigo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *