Kimbunga Maria kimekata umeme katika kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu zaidi ya milioni 3.5 huku kikiharibu vibaya makazi ya watu katika kisiwa hicho.

 Kimbunga hicho hatari kutokea duniani, imeripotiwa kwa sasa kimeondoka nchini Puerto Rico na kupunguza nguvu zake.

Baada ya kimbunga Maria kuipiga Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia majumbani mwao kuanzia jana saa 12 jioni na hadi saa 12 asubuhi.

Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hiyo. Hi ni hatua ya kuwazuia watu kupata ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka na vifuzi vilivyo barabara za mji.

Mapema Rossello alimuomba Rais Donald Trumo kukitangaza kisiwa hicho kuwa eneo la janga baada ya kimbunga kusababisha mafuriko makubwa na upepo unaotishia maisha.

Alisema kuwa kuna uwezekano wa uharibu mkuwa licha ya vitisho 500 kubuniwa kuwalinda watu. Kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 7 katika kisiwa cha Dominica ambacho kiliathiriwa vibaya siku ya Jumatatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *