Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Diane Rwigara amemtaka Rais Paul Kagame kumuachilia yeye, mamake na dadake.

Akiwa mahakamani, Bi Rwigara amesema kwamba serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Wanawake hao watatu, ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi tuhuma ambazo wameziita zenye mrengo wa kisiasa.

Bi Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa Rwanda, Uchaguzi ambao Bwana Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *