Kiongozi wa upinzani nchini DR Congo Etienne Tshisekedi ameelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu ya kiafya.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo chama chake kinaendelea na mazungumzo ya kugawana mamlaka kufuatia hatua ya rais Joseph Kabila kukataa kujiuzulu baada ya muda wake wa kuhudumu kumilizika mwezi uliopita.

Viongozi wa kanisa la Katoliki nchini humo walifanikiwa kuweka makubaliano ambapo bwana Tshisekedi alitarajiwa kupewa wadhfa wa serikali ya mpito hadi pale uchaguzi utakapofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Kutokana na sababu hizo za kutotoka madaraka kwa rais Kabila wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakaanza kuandamana wakishindikiza kuondoka madaraka kwa rais wa taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *