Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, George Mbijima amemtaka Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mriro Jumanne kumuweka rumande Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Bruno Minja kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kazi na kumuachia Mganga Mfawidhi.

Agizo hilo lilitolewa na kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge muda mfupi baada ya kukabidhiwa kwa Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri katika kijiji cha Bukooba wilayani hapa tayari kwa kuanza mbio zake katika mkoa wa Shinyanga juzi.

Kiongozi huyo aliamuru kukamatwa kwa Mganga Mkuu huyo wa Hospitali ya Mji wa Kahama, Minja katika tukio la Mradi wa kwanza wa kufungua zahanati ya Isagehe iliyopo kata ya Isagehe ambapo Mganga mkuu huyo alihitajika kuwepo katika uzinduzi huo, baadala yake kumuachia jukumu hilo Mganga Mfawidhi, Joseph Ngowi.

Mbijima baada ya kufika katika zahanati hiyo kwa ajili ya ufunguzi na kuweka jiwe la msingi, alipohoji kuhusu kuwepo kwa Mganga Mkuu kwa ajili ya kutoa kitabu cha kusaini wageni hakuweza kupatikana kwa wakati huo, badala yake kazi hiyo alimuachia Mganga Mfawidhi ambaye pia alishindwa kutekeleza wajibu wake na kubaki kutetemeka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Underson Msumba akizungumzia sakata la kukamatwa na kuweka ndani kwa Mganga Mkuu huyo, alisema alifanya kosa kubwa kumuachia majukumu Mganga Mfawidhi shughuli nzima ya kitaifa huku akitambua kuwa mhusika mkuu ni yey

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *