Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne wilayani Kibiti, Iddy Kirungi ameuawa kwa kupigwa risasi.

Mauaji hayo yametokea katika kijiji cha Muyuyu Kata ya Mtunda wilayani Kibiti  mkoani Pwani.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo.

Amesema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia kutokana na watu hao kwenda kwake.

Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.

Mganga wa zamu katika kituo cha afya Ikwiriri, Dk Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.

Amesema majeruhi huyo walimpatia rufaa kwenda Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *