Tume huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo imetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo sasa utafanyika Novemba mwaka wa 2018 na wala sio mwaka huu kama ilivyotarajiwa.

Viongozi kadha wa upinzani walioshiriki katika mazungumzo ya amani ya kitaifa wameafikiana na uamuzi huo, lakini kuna wale wanaoupinga wakisema ni njama ya Rais Joseph kabila kusalia madarakani.

Uchaguzi nchini Congo ulitarajiwa kufanyika mwaka huu kama katiba ya nchi hiyo inavyosema lakini sasa umegharishwa mpaka mwaka 2018 baada ya makubaliano ya pande ya serikali na upinzani.

Mwezi uliopita nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliingia katika machafuko mara baada ya tume ya uchaguzi kurangaza kwamba uchaguzi wa nchi hiyo hutofanyika mwaka huu mpaka utakapangwa tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *