Aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru ameviambia vyama vya upinzani nchini visahau kushinda uchaguzi mkuu ujao kama hakutakuwa na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.

Kingunge amesema hayo baada ya Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akichukua nafasi ya Jaji Damian Lubuva aliyestaafu.

NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *