Ni wazi kuwa mwaka jana mchuano wa nani mkali zaidi kati ya mastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba ulimalizika kwa kushindanishwa vitu vingi huku Diamond Platnumz akimfunika Kiba kwa wingi wa tuzo.

Lakini Kiba nae akaonyesha jeuri kubwa ya ubora wa nyimbo ambapo ngoma yake AJE ikafanikiwa kutwaa tuzo nyingi zaidi ya ngoma yoyote hapa Bongo.

Sasa baada ya Diamond Platnumz kuweka wazi mipango yake kupitia mtandao wa INSTAGRAM kuwa mwaka huu ana mipango KIBAO…Kiba ameanza kutekeleza kile anachoamini ni ‘World Tour’.

Staa huyo anaanza na ziara yake nchini Afrika Kusini kisha ataelekea kwenye mataifa ya Magaharibi ikiwemo Marekani na barani Ulaya.

Hebu cheki kionjo cha tour hiyo ya South Africa.

Je, baada ya kuachia ‘Marry You’, Platnumz atakuja na kitu gani kumfunika King?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *