Staa wa miondoko ya Hip-Hop kutokea Kenya, King Kaka amewajia juu na kuwatupia lawama mapromota nchini humo kwa kuwalipa fedha chache wasanii wa ndani na kuwalipa fedha nyingi wasanii wa nje.

King Kaka ametoa malalamiko hayo kwenye mtandao wa Facebook na kuwatolea mfano Diamond na Alikiba ambao wamekuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi kila wakitumbuiza nchini humo.

rabit

Kupitia ukurasa wake wa Facebook King Kaka ameandika “Alikiba na Diamond wanalipwa 2million sio mbaya lakini wasanii wa kenya wanapewa 300k, 400k ata unaweza Pata mi 100k (shame, what a shame) sahizo bado yule amekupa show anataka cut yake which sio mbaya but what do fans expect”.

Msanii huyo amedai kuwa wasanii wa Kenya hawapewi heshima wanayostahili na hivyo kudidimiza muziki wa nchi hiyo kutokana na ukandamizaji huo unaoendelea katika muziki nchini Kenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *