Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jana alionekana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Msingi ya Lucky Vicent.

Kinana hajaonekana hadharani tangu kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Machi 12 mjini Dodoma.

Na maswali yalipoanza kuhusu kutoonekana kwake, Rais John Magufuli alisema ÔÇťamemtuma India kwenda kutibiwa.

Jana, Kinana, ambaye amewahi kuwa mbunge wa Arusha na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, alionekana mjini hapa na alitumia muda mwingi kusalimiana na watu waliokuwa wakimfuata.

Kinana alifika uwanjani akiwa kwenye gari la ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha na alipanda moja kwa moja jukwaa kuu na baadaye alipata muda wa kusalimia mamia ya watu waliokuwa wamefurika katika uwanja huo.

Wakati shughuli za kuaga miili ikiendelea, Kinana aliteta kwa dakika chache na Lowassa aliyekuwa ameongozana naye.

Lowassa alisikika akimuuliza Kinana kuhusu afya yake na alijibiwa na katibu mkuu huyo wa CCM kuwa anaendelea vizuri. Wawili hao waliendelea na mazungumzo, huku wakipigwa picha.

Baadaye Kinana alizungumza na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia alimpa pole.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *