Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ndugu Abdurhaman Kinana amesema mabadiliko wanayoyafanya ndani ya chama hicho yatakuwa yanagusa sehemu muhimu kama Katiba ndani ya CCM, kanuni za uchaguzi pamoja na kanuni za Jumuiya.

Hayo aliyabaanisha katika mkutano Maalum wa mabadiliko uliofanyikia Jijini Dodoma, huku akibainisha baadhi ya vitu na kusema mageuzi hayo hayamlengi mtu wala kikundi chochote bali yanalenga kutoa ufanisi ndani ya chama hicho.

Kinana amesema kuwa“CCM imekuwa na utamaduni wa mabadilko na imeshafanya hivyo mara 15 na awamu hii ni mara ya 16 sasa dhamira ikiwa ni kuweka uhai, ubora na ushindi wa CCM”.

Aidha Katibu huyo ametaja mabadiliko waliyoyakusudia kuyafanya kuwa ni kupunguza utitiri wa vyeo, idadi ya vikao viwe vichache ambavyo vitakuwa na tija kwao pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe.

Kwa upande mwingine Kinana amefananisha mabadiliko hayo na vyama vingine vikongwe duniani ikiwemo chama cha Kikomunist cha China ambacho wanachama wengi lakini idadi ya wajumbe wa mikutano yao wakiwa wachache pamoja na chama cha African National Congress (ANC) cha nchini Afrika ya Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *