Mwanamuziki nyota nchini Kenya, Victoria Kimani amesema kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuwashirikisha wasanii wa mbali katika kazi zake kikubwa ni kufanya kazi bora zaidi.

Desemba 4, mwaka huu, msanii huyo ameachia albamu yake ya kufungia mwaka ijulikanayo kwa jina la ‘Safari’, huku akidai kuwa hajawashirikisha wasanii wengi kutoka mbali kwa kuwa anaamini ubora wa albamu unatokana na ubora wa kazi.

Kimani amesema kuwa “Nimeachia albamu yangu ya Safari, sijawashirikisha wasanii wengi kutoka mbali kwa kuwa ninaamini mwenyewe naweza kuifanya albamu kuwa bora.

Kimani amesema ameongeza kwa kusema kuwa siku zote ubora wa albamu unatokana na ubora wa nyimbo zilizopo na siyo kushirikisha wasanii wenye majina makubwa.

Baadhi ya wasanii ambao wapo kwenye albam yake mpya ni Michael Addo ‘Sarkodie’ kutoka nchini Ghana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *