Mwanamitindo nyota wa Marekani, Kim Kardashian na mumewe Kanye West wamethibitisha kwamba watapata mtoto mwengine kutoka kwa mama anayebeba mimba kwa niaba yao.

Kumekuwa na ripoti nchini Marekani kwamba dadake mdogo Kim , Khloe pamoja na dada wa kambo Kylie Jenner pia ni wajawazito.

Kim ambaye ameolewa na rappa Kanye West amekuwa akizungumza katika kipindi hicho kuhusu matatizo aliyonayo kushika mimba.

Ametaja ripoti za awali kwamba amekuwa akisubiri kuwa na mtoto kutoka kwa mama atakayebeba mimba kwa niaba yake kama uongo.

Mnamo mwezi Juni, wanandoa hao walidaiwa kukodisha mwanamke atakayebeba uja uzito kwa niaba yao kutokana na matatizo ya kiafya yaliotokana na watoto wawili wa Kim Kardishian.

Iwapo itathibitishwa atakuwa mtoto wao wa tatu baada ya North, Four na Saint ambaye atakuwa na miaka miwili mwezi Disemba.

Ripoti kadhaa za habari wiki iliopita zimesema kuwa Khloe kardashian , 33 na Kylie Jenner 20 ni waja wazito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *