Nyota wa televisheni nchini Marekani Kim Kardashian ameshambuliwa na kuzuiliwa na watu waliokuwa na silaha katika hoteli moja mjini Paris nchini Ufaransa.

Msemaji wake anasema nyota huyo wa uigizaji wa vipindi vya maisha ya uhalisia alizuiliwa na watu waliokuwa wamejifanya maafisa wa polisi ambao walikuwa wamejifunika nyuso zao.

Kanye West amekatisha ghafla tamasha ambayo amekuwa akishiriki mjini New York kutokana na tukio hilo alilofanyiwa mke wake.

Kanye West alikuwa akitumbuiza katika tamasha ya Meadows Music and Arts Festival na amesitisha ghafla utumbuizaji na kuwaambia mashabiki kwamba alikuwa na matatizo ya kifamilia.

Kardashian West alikuwa ameenda Paris, pamoja na mamake Kris Jenner na dadake Kendall Jenner, kuhudhuria maonyesho ya mitindo.

Haijabainika iwapo watoto wa wawili hao, North mwenye umri wa miaka 3 na Saint mwenye umri wa miezi 10, walikuwa kwenye hoteli hiyo na Kardashian.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *