Mwanamitindo nyota wa Marekani, Kim Kardashian ameshtaki tovuti moja ya udaku kuhusu wasanii kwa kudai kwamba aliigiza kisa cha wizi mjini Paris wiki iliyopita.

Kwenye kesi hiyo, anataka alipwe kiasi cha pesa ambacho hakijafichuliwa kwa kuharibiwa jina.

Ameshtaki tovuti ya MediaTakeout, pamoja na mwanzilishi wake, Fred Mwangaguhunga.

Nyota huyo alifungwa mikono na majambazi waliokuwa na bunduki ambao waliingia kwenye chumba chake hotelini Paris mapema mwezi huu, polisi wanasema.

Wezi hao walitoroka na vito vya vya thamani vyenye thamani  ya $10m (£8m)

Kardashian mwenye umri wa miaka 35 ameolewa na mwanamuziki Kanye West na wamejaliwa watoto watatu. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye televisheni cha Keeping up with the Kardashians.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *