Mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian amesema ameingiwa na hofu na kuomba msaada wa kisaikolojia kuhusu kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Zika unaosambaa kwa kasi katika Bara la Amerika.

Kim Kardashian amesema hayo wakati akifanya kipindi chake cha televisheni cha “keeping Up with the Kardashians” baada ya kuonekana kuwa na hofu kubwa moyoni mwake kuhusu kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Kardashian alisema haya wakati akifanya kipindi chake hiko “Ninashangaa, itakuwaje kama tukifanyiwa vipimo na nikagundulika nimeambukizwa Zika kabla hatujaudi nyumbani?”.

Kim na Kourtney wapo nchini Cuba na watoto wao pamoja na  Kanye West, Khloe Kardashian and Malika Haqq na msaidizi wao Stephanie wote walionekana kuwa na wasiwasi kuhusu afya ya kila mmoja wao endapo watapimwa huko ugenini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *