Ndoa ya mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian na mume wake Kanye West uhenda ikafika mwisho baada ya Kim Kardashian kudai talaka.
Wawili hao wameripotiwa kuelekea kutengana na hata Kim Kardashian kudai talaka yake baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka miwili na nusu.
Kwa mujibu wa Us Weekly Kim Kardashian ametajwa kuwa yeye ndio anataka talaka hii na itakuwa talaka yake ya tatu baada ya kuachana na Damon Thomas na mcheza kikapu Kris Humphries.
Watu wa karibu na Kim K wanasema ni kweli ana taka talaka na haki zote za malezi ya watoto wao wawili ambao ni North ‘3’ na Saint mwenye mwaka mmoja.
Kim K amekaa mbali na Kanye West kwa muda sasa toka aruhusiwe kutoka hospitalini baada ya kupata matatizo ya akili na msongo wa mawazo.